# Mpe Mungu baraka ... acha sauti ya sifa yake isikike Misemo hii miwili ina maana za kufanana. Wazo linarudiwa kusisitiza umuhimu wa kumsifu Mungu. # yetu Katika mstari huu "yetu" inajumuisha Daudi na watu anaozungumza nao. # haruhusu miguu yetu kuteleza Mwandishi anazungumzia ulinzi wa Mungu kama kuwaepusha watu wake kuteleza wanapotembea au kuanguka katika mteremko wa ghafla. "hajaturuhusu kuanguka katika maafa"