# mwamba wa nguvu yangu na kimbilo langu liko katika Mungu Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni mwamba unaomlinda mtu dhidi ya adui zake. Anamzungumzia Mungu pia kana kwamba ni kivuli kinachotoa ulinzi. "Mungu huwa ananipa nguvu na ulinzi" # mwaga moyo wako Hii inamaanisha kumwambia Mungu hisia zako za ndani kana kwamba ni kumwaga kimiminiko. "mpe Mungu mawazo yako ya ndani" # kimbilio letu Neno "letu" linamaanisha Daudi na watu anaozungumza nao.