# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Mungu wa nguvu yangu Maana zinazowezekana ni 1) "Mungu unayenilinda" au 2) "Mungu unayenipa nguvu" # Kwa nini umenikataa? Kwa nini ninaomboleza kwa sababu ya ukandamizaji wa adui? Mwandishi anauliza maswali haya ili kulalamika kwa Mungu na kuonesha hisia yake, sio kupata jibu. # Kwa nini ninaomboleza "Kuomboleza" ni kufanya matendo yana onesha kuwa na huzuni sana. # kwa sababu ya ukandamizaji wa adui Neno "ukandamizaji" linaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "kwa sababu adui zangu wananikandamiza"