# Taabu zisizoweza kuhesabika zinanizunguka Hapa taabu zinazungumziwa kana kwamba ni vitu vinavyomzunguka na kumtega mwandishi. "kuna taabu nyingi zimenizunguka kuliko navyoweza kuhesabu" au "taabu nyingi huja kwangu kuliko navyoweza kuhesabu" # zisizoweza kuhesabika Hii imeelezwa katika hali hasi kuweka mkazo wa idadi. "zilizo nyingi kwa idadi" # udhalimu wangu Hii inamaanisha matokeo ya dhambi. "matokeo ya udhalimu wangu" # umenishika Udhalimu wa mwandishi unazungumziwa kana kwamba ni adui zake wanaomdhuru. # siwezi tena kuona kitu Matoleo yanatofautiana katika kuelewa msemo huu. Inaweza kuwa inamaanisha kuwa mwandishi analia sana hadi hawezi kuona chochote kwa sababu ya machozi yake. # moyo wangu umeshinda Hapa "moyo" inamaanisha ujasiri wa ndani wa mwandishi.