# Adui wa Yahwe watakuwa kama utukufu wa malisho Mwandishi analinganisha adui wa Yahwe na maua yanayo chanua katika mashamba. # watateketezwa na kupotea katika moshi Mwandishi anazungumzia uharibifu wa waovu kwana kwamba ni magugu au maua yaliyo nyauka shambani yanayochomwa baada ya mavuno. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atawaangamiza kama moto unavyogeuza magugu ya shamba kuwa moshi" # ni mkarimu na hugawa Hizi zina maana moja na zinasisitiza ukarimu wa wenye haki.