# mifupa yangu ilikuwa inachakaa Hapa "mifupa yangu" inamaanisha mwandishi. "nilikuwa nachakaa" au "nilikuwa nakuwa mdhaifu" # siku nzima Lahaja hii inamaanisha "endelevu." "wakati wote" # mchana na usiku Tofauti hizi zinajumlisha kila kitu katikati. "wakati wote" # mkono wako ulikuwa mzito juu yangu Hapa "mkono" inamaanisha Yahwe. Msemo wote ni lahaja inayomaanisha "umenitesa." "umenifanya niteseke sana" # Nguvu yangu ilinyauka kama kwenye ukame wa majira ya joto Nguvu ya Daudi inalinganishwa na mmea mdogo wa kijani unaogeuka kuwa wa rangi ya kahawia na kuanguka katika majira ya kiangazi. # Sela Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kihebrabia, na zingine haziliweki.