# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Kwa mwanamuziki mkuu "Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu" # Zaburi ya Daudi Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi. # Katika wewe Yahwe, ninakukimbilia Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi inazungumziwa kama kumkimbilia. "Naenda kwako Yahwe, kwa ajiliya ulinzi" # usiniache niaibike kamwe Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "usiwaache wengine waniaibishe" # uwe mwamba wangu wa kukimbilia; ngome ya kuniokoa Mseno "uwe mwamba wangu wa kukimbilia" ni ombi kwa ajili ya ulinzi. Msemo wa pili unawekea mkazo msemo wa kwanza. # mwamba wangu wa kukimbilia Yahwe anazungumziwa kana kwamba yeye ni mwamba mkubwa ambao utamlinda mwandishi na mashambulio. "kama mwamba mkubwa ambao nitakuwa salama" # ngome ya kuniokoa Yahwe anazungumziwa kana kwamba yeye ni ngome imara ambayo mwandishi anaweza kulindwa dhidi ya adui zake.