# Kauli Unganishi: Mwandishi anaendelea kuelezea nguvu ya sauti ya Mungu. # Anaifanya Lebanoni kurukaruka kama ndama Lebanoni inazungumziwa kana kwamba ni ndama mchanga. Hii inasisitiza kwamba Yahwe akizungumza, nguvu ya sauti yake hutikisa ardhi. "Hufanya nchi ya Lebanoni kutikisika kama ndama anaye rukaruka" # kurukaruka kuruka kidogo hapa na pale # Sirioni kama kama ng'ombe mdogo Sirioni inazungumziwa kana kwamba ni ng'ombe mchanga. Hii inasisitiza kuwa Yahwe akizungumza, nguvu ya sauti yake hutikisia ardhi. "Huifanya Sirioni kuruka kama ng'ombe mchanga" # Sirioni Huu ni mlima Lebanoni. Pia unaitwa mlima Hermoni. # Sauti ya Yahwe inatuma miali ya moto Sehemu zote zenye "sauti" zinamaanisha Yahwe anazungumza. "Yahwe akizungumza husababisha miali ya radi kuonekana angani" # miali ya moto hii inamaanisha mwale wa radi.