# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Zaburi ya Daudi Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi. # wana wa Mungu Msemo "wana wa" ni njia ya kusema "kuwa na sifa za." "nyie watu hodari" # Mpeni sifa kwa Yahwe kwa utukufu wake na nguvu Nomino dhahania ya "utukufu" na "nguvu" zinaweza kuelezwa kama vitenzi. "Mpeni heshima Yahwe kwa kuwa ana utukufu na nguvu" # Mpeni Yahwe utukufu ambao jina lake linastahili Nomino dhahania ya "heshima" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "Mheshimu Yahwe kama ambavyo jina lake linastahili" au "Tangazeni kuwa Yahwe ni mtukufu kama jina lake linavyostahili" # ambao jina lake linastahili Msemo "jina lake" unamaanisha Yahwe au sifa yake. "kama ilivyo sahihi kwa sababu alivyo"