# Usiufiche uso wako kwangu Uso unawakilisha usikivu wa Yahwe. Msemo "Usiufiche uso wako" ni njia kumwomba Mungu asimkatae. "Usinikatae" au "Usiache kunitunza" # usimgeuza mtumishi wako kwa hasira Daudi alisema "mtumishi wako" kumaanisha ni yeye mwenywe kwa njia ya unyenyekevu. "usinikasirikie" # usiniache wala kunitupa Maneno "kuacha" na "kutupa" yana maana sawa. Mwandishi anasisitiza kuwa hataki Mungu amuache. # wala kunitupa "na usinitupe" au "na usiniache" # Mungu wa wokovu wangu Nomino dhahania ya "wokovu" inaweza kuelezwa kama "okoa." "Mungu anayeniokoa" au "kwa kuwa wewe ni Mungu unayeniokoa" # Hata kama baba na mama yangu wakiniacha Hasemi kuwa kweli wamefanya hivi au kwamba watafanya hivi. Wazo lake ni kwamba hata kama wangefanya hivyo, Mungu asingemuacha. # Yahwe atanichukua "Yahwe atanitunza"