# Sikia, Yahwe, sauti yangu Hapa "sauti" inamaanisha kuwa mwandishi anasema. "Nisikie, Yahwe" # nijibu Hii inaashiria kuwa Yahwe anasikia maombi ya mwandishi na Yahwe atafanya kile mwandishi anachoomba. "jibu ombi langu" au "fanya ninachokuomba" # Moyo wangu unasema Hapa "moyo" unawakilisha akili na mawazo ya mtu. "Moyoni mwangu nasema" au "Ninajiambia" # Utafute uso wake Mtu kwenda hekaluni kumwomba Yahwe inazungumziwa kana kwamba mtu huyo anamtafuta Yahwe. "Hapa "uso" unamwakilisha Mungu. "Nenda ukaombe kwa Yahwe" # Nautafuta uso wako, Yahwe Mtu kwenda hekaluni kumwomba Yahwe inazungumziwa kana kwamba mtu huyo anamtafuta Yahwe. "Hapa "uso" unamwakilisha Mungu. "Nitakuja kwenye hekalu lako na kuomba kwako"