# katika siku ya taabu Hapa "siku" inawakilisha muda mrefu zaidi. "katika wakati wa taabu" au "ninapokuwa na taabu" # atanificha "atanilinda" # kivuli chake ... hema lake Zote hizi zinamaanisha hema ambamo mwandishi anamwabudu Mungu. # katika mfuniko wa hema lake Neno "mfuniko" inawakilisha kitu kinachoficha na kulinda. # Ataniinua juu ya mwamba Mungu kumweka salama mwandishi kutoka kwa adui zake inazungumziwa kanakwamba Mungu alimuweka katika mwamba wa juu ambapo adui zake hawakuweza kumfikia. # kichwa changu kitainuliwa juu ya adui zangu Hii inawakilisha mwandishi kupokea sifa au heshima anapowashinda adui zake. Inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu wataniheshimu nitakaposhinda pambano langu dhidi ya adui zangu" au "Mungu atanipa heshima kwa kuniwezesha kuwashinda adui zangu"