# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Zaburi ya Daudi Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi. # Nimetembea Neno "kutembea" ni sitiari ya tabia. "Nimeenenda" # Yahwe Matumizi ya mtu wa tatu wa "Yahwe" inaweza kuelezwa katika hali ya mtu wa pili. "wewe" # bila kuyumba Mashaka yanazungumziwa kana kwamba ilikuwa ni kuyumba na kupepea mbele na nyuma. "bila kuwa na shaka" # Nichunguze "Nijaribu" # jaribu usafi wa sehemu zangu za ndani na moyo wangu Hapa "sehemu za ndani" na "moyo" inamaanisha nia. "jaribu kama nia zangu ni nzuri" # Kwa kuwa uaminifu wako wa agano uko mbele ya macho yangu Hapa "macho" yanawakilisha mawazo ya mtu. "Kwa kuwa huwa nawaza kuhusu jinsi ulivyo mwaminifu kwangu kwa sababu ya agano lako" # ninatembea katika uaminifu wako Neno "kutembea" ni sitiari ya tabia. "Ninaendesha maisha yangu kulingana na uaminifu wako" au "Ninaenenda jinsi nilivyo kwa sababu ya uaminifu wako"