# Hakika wema na uaminifu wa agano utanifuata Yahwe kuwa mwema na mwaminifu kwa mtu inazungumziwa kana kwamba wema na uaminifu wa agano ni vitu vinavyomfuata mtu. "Hakika utakuwa mwema na mwaminifu kwangu" # siku zote za maisha yangu Nomino dhahania ya "maisha" inaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "maadamu nina ishi" # nyumba ya Yahwe Maana zinazowezekana ni kwamba 1) hii inamaanisha nyumba ya milele ya Yahwe, au 2) hii inamaanisha hekalu la Yahwe Yerusalemu. # kwa muda mrefu sana Maana zinazowezekana ni 1) "milele" au 2) "maadamu nina ishi."