# Walidhulumiwa watakula na kuridhika Hii inamaanisha mlo wa ushirika unaotokea baada ya mwandishi kumpa Mungu sadaka alizoahidi. Atawakaribisha wale waliokuwa wanateseka kula sehemu ya mnyama aliyemtoa sadaka. # wale wanaomtafuta Yahwe Wale wanaotaka kumjua Yahwe na kumpendeza wanazungumziwa kana kwamba wanamtafuta Yahwe kwa uhalisia. # Mioyo yenu iishi milele Hapa "mioyo" inawakilisha mtu mzima. "Na uishi milele" # Mioyo yenu Hapa "yenu" inamaanisha watu walio dhulumiwa. # watakumbuka na kumgeukia Yahwe Kuanza kumtii Yahwe kunazungumziwa kana kwamba watu wanamgeukia Yahwe kimwili. "watamkumbuka Yahwe na kumtii" # familia zote za mataifa zitasujudu chini mbele yako Hii inamaanisha kitu kimoja na sehemu ya kwanza ya sentensi. Mwandishi anasisitiza kuwa kila mtu kutoka kila sehemu atamwabudu na kumtii Yahwe. # zitasujudu chini mbele yako Hii ni alama ya kumpa utkufu na heshima mtu. # mbele yako Hapa "yako" inamaanisha Yahwe. Inaweza kutafsiriwa katika hali ya mtu wa tatu ili ilingane na sehemu ya kwanza ya sentensi. "mbele yake"