# walikusudi "walipanga." Waliopanga ni adui wa Mungu na mfalme. # maovu dhidi yako "kufanya vitu viovu" # wakatunga njama "wakafanya mpango" au "wakiunda hila" # Kwa kuwa utawageuza; utachukua upinde wako mbele yao Maana zinazowezekana za anaye zungumziwa ni 1) mfalme au ni 2) Mungu na zinamzungumzia kana kwamba alikuwa ni shujaa mwenye upinde na mishale. # utawageuza Hii ni njia ya kusema kuwa Mungu na mfalme watawashinda adui zao vitani. # utachukua upinde wako mbele yao Hii inaashiria kuwa anawapiga adui zake kwa mishale.