# Muweke mtumishi wako pia mbali na Lahaja hii inaonesha mtumishi kama ametolewa kwenye dhambi ambazo hataki kutenda. "Pia, mlinde mtumishi wako kutokufanya" au "Pia, hakikisha sifanya" # mtumishi wako Daudi anajiita "mtumishi wako" anapozungumza na Mungu kama ishara ya heshima. "mimi" # usiziache zinitawale Dhambi zinaelezwa kana kwamba ni mfalme anayeweza kutawala juu ya mtu. "usiache dhambi zangu ziwe kama mfalme anayetawala juu yangu" # sina hatia na makosa mengi "sina hatia ya kuasi dhidi yako" au "sina hatia ya kutenda dhambi nyingi" # maneno ya mdomo wangu na mawazo ya moyo wangu Misemo hii pamoja inaeleza kile ambacho mtu anasema na kuwaza. "vitu ninavyosema na vitu ninavyowaza" # yakubalike machoni pako "yapokee kukubaliwa machoni pako" au "yakupendeze wewe" # machoni pako Hii inamaanisha Mungu mwenyewe. "kwako" # Yahwe, mwamba wangu Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni mwamba ambao mtu anaweza kupanda kujilinda dhidi ya adui zake. "Yahwe, wewe ni kama mwamba wangu"