# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Kwa mwanamuziki mkuu "Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu" # Zaburi ya Daudi Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi. # Mpumbavu husema moyoni mwake Hii ni lahaja inayomaanisha kuzungumza mwenyewe au kujiwazia mwenyewe. "Mtu mpumbavu anajiambia" # Wameharibika walioharibika inaashiria binadamu wapumbavu wanaosema hakuna Mungu.