# Asema Anayesema ni mtu mwovu na watu waovu kwa ujumla. # Mungu amesahau Kukataa kuzingatia kile ambacho watu wanafanya inazungumziwa kama kusahau. "Mungu hazingati" au "Mungu hajali kuhusu kile nachofanya" # anafunika uso wake Kukataa kuzingatia kitu ambacho mtu anafanya kama kufunika uso wa mtu. "Mungu anakataa kuona kinachotokea" # hatahangaika kutazama Kuzingatia kile ambacho mtu anafanya inazungumziwa kama kukiangalia. "hatahangaika kuzingatia" au "hatajali" # Inuka Kuanza kufanya kitu inazungumziwa kama kuinuka. "Fanya kitu" # Inua mkono wako Hapa kuinua mkono kumpiga mtu inaashiria kumwadhibu. "kumpiga kwa nguvu" au "kumwadhibu mtu mwovu"