# Anasema "Mtu mwovu anasema" # katika vizazi vyote Hii inaweza kumaanisha "milele." # sitakutana na taabu Kupitia taabu inazungumziwa kama kukutana nayo. "Sitakuwa na shida zozote" # Mdomo wake umejaa laana na maneno ya uongo na ya kudhuru Kile watu wanachosema kinazungumziwa kama kuwa mdomoni mwao. "huwa anawalaani watu na kusema vitu ambavyo ni vya uongo na vya kudhuru" au "Huwa analaani watu, kusema uongo, na kutishia kuwadhuru watu" # ulimi wake huumiza na kuangamiza Hapa ulimi unaashiria kuongea. au "kile anachokisema kinaumiza na kuangamiza watu" au "anazungumza maneno yanayowatisha na kuumiza watu"