# imetaabika sana "ogopa" au "wasiwasi" # hii itaendelea hadi lini? Daudi anatumia swali hili kuonesha kuwa hataki kuendelea kujisikia mdhaifu na mwenye taabu. "tafadhali, usiruhusu hii iendelee!" # Rudi, Yahwe Daudi anazungumzia Mungu kumtendea wema kama Mungu kurudi kwake. "Yahwe, rudi kwangu" au "Nione huruma, Yahwe" # Kwa kuwa katika kifo hakuna kumbukuku lako. Nani atakupa shukrani kuzimu? Sentensi hizi mbili zina maana ya kufanana. # Kwa kuwa katika kifo hakuna kumbukuku lako. Kumbukumbu inaashiria sifa. "Kwa kuwa watu wanapokufa, hawakusifu tena" # Nani atakupa shukrani kuzimu? Daudi anatumia swali hili kusisitiza kuwa hakuna mtu anayetoa shukrani kwa Mungu toka kuzimu. "Hakuna mtu kuzimu atayekupa shukrani!" au "Wafu hawawezi kukusifu"