# wote wanaokukimbilia wafurahi Mungu anazungumziwa kana kwamba ni kambi, sehemu ambayo watu wanaweza kulindwa. "Wote wanaokuja kwako kwa ulinzi wafurahi" # wote wanaokukimbilia wafurahi ... wapige kelele za shangwe kwa sababu unawalinda Vishazi hivi viwili vina wazo la kufanana. # wanaokukimbilia Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi kunazungumziwa kama kumkimbilia yeye. "kwenda kwako kwa ulinzi" # wale wanaolipenda jina lako Jina la Mungu linamwakilisha yeye. "wale wanaokupenda" # utawazunguka na fadhila kama ngao Fadhila za Mungu zinazungumziwa kama ngao. "utawaonesha fadhila na kuwalinda kama askari wanavyojilina kwa ngao" au "kwa sababu u mkarimu kwao, utawalinda"