# Kauli Unganishi: Yahwe anaendelea kuzungumza na mfalme mpya wa Israeli. # mataaifa kwa urithi wako ... sehemu za mbali za nchi kwa mali yako Mafungu haya yanaonesha mawazo ya kufanana sana. # sehemu za mbali za nchi "ardhi iliyo mbali kabisa" # Utawavunja kwa fimbo ya chuma; kama chupa ya mfinyanzi, utawaponda vipande vipande. Vifungu hivi vinanaonesha mawazo ya kufanana sana. # Utawavunja kwa fimbo ya chuma Kuyashinda mataifa inazungumziwa kama kuyavunja, na nguvu yake inazungumziwa kama fimbo ya chuma. "Utawashinda kabisa kwa nguvu yako" # utawaponda vipande vipande Kuangamiza mataifa inazungumziwa kana kwamba yanaweza kupondwa kama chupa ya udongo. "utawaangamiza kabisa kama chuma ya udongo" # chupa ya mfinyanzi Mfinyanzi ni mtu anayetengeneza vyungu vya udongo na chupa. Hizi ni nyepesi kuvunjika. "chupa ya udongo" au "chungu cha udongo"