# Yeye ... Bwana Maneno haya yanamaanisha Yahwe. Yahwe mara nyingi huitwa "Bwana" lakini maneno kwa ajili ya "Yahwe" na "Bwana" ni tofauti. # aketiye mbinguni Hapa kuketi inamaanisha kutawala. Kile anachokalia kinaweza kuelezwa vizuri. "anatawala mbinguni" au "anaketi katika kiti chake cha enzi mbinguni" # Bwana anawadhihaki "Bwana anawadhihaki hao watu." Kwa nini anawadhihaki inaweza kuelezwa vizuri. "Bwana anawadhihaki kwa mipango yao yakipumbavu" # na kuwatisha katika gadhabu yake "gadhabu" inamaanisha kuwa na hasira kali. # kuwatisha "kuwaogofya"