# Maelezo ya Jumla Baba anamfundisha mtoto wake kwa kutumia shairi. # kama utapokea maneno yangu Hapa "maneno" yanawakilisha mafundisho " kama utasikiliza ambacho ninakufundisha" # kama utapokea Huu ni mfululizo wa kauli zenye mashariti zinazofika tamati katika 2:5 # zihifadhi amri zangu ndani yako " zihesabu amri zangu kuwa za thamani kama hazina" # masikio yako yawe na usikivu kwa ajili ya hekima na kuelekeza moyo wako kwenye ufahamu "kama masikio yako yatakuwa masikivu kwa ajili ya hekima na kuelekeza moy wako kwenye ufahamu" # masikio yako yawe na usikivu "Jilazimishe kusikiliza kwa umakini wewe mwenyewe" # Hekima "sikiliza mabo ya busara ambayo ninakufundisha" # elekeza moyo wako kwenye ufahamu "jitahidi sana kufahamu maana ya busara"