# Maelezo ya Jumla Hekima anaendelea kuongea. # Sikiliza "kusikiliza kwa umakini" # Mimi nitamimina mawazo yangu kwenu Hekima anawaambia watu kila kitu anachofikiri juu yao, mawazo yake yanaongelewa mithili ya kimiminika ambacho anaweza kuwamiminia. # Mimi nitafanya maneno yangu yajulikane kwenu " Nitawaambia yale ninayoyafikiria" # Mimi nimeunyosha mkono wangu Hii ni nahau maana yake " Nimewaalikeni kuja kwangu"