# pia ni kuwapa hekima wajinga ' pia kuwafunza wale ambao ni wajinga namna ya kuwa na busara" # wajinga "bila uzoefu, isiyo kamavu/uchanga" # kuwapa maarifa na busara vijana "na kuwafunza vijana wanachohitaji kufahamu na jinsi ya kutambua jambo zuri la kufanya" # busara kufahamu kinachopaswa kufanyika katika mazingira husika. # Watu wenye busara wasikie na kuongeza elimu yao "Wale wenye busara wazingatie na kujifunza zaidi" # watu wenye ufahamu wapate mwongozo "watu wenye ufahamu wajifunze kwa methali hizi jinsi ya kufanya maamuzi mazuri" # vitendawili misemo ambayo mtu anaweza kuifahamu baada tu ya kutafakari juu yake.