# Sentensi Unganishi: Paulo anazungumzia kuhusu waamini wa Filipi wamekuwa wakimsaidia kifedha na kumalizia na salam na shukran. # kuridhika "kutosheka" au "kufurahi" # katika mazingira yote "haijalishi mazingira niliyo nayo" # Nafahamu kuishi katika hali ya kupungukiwa...kuwa na vingi Paulo anajua jinsi ya kuishi maisha ya furaha aidha akiwa hana au akiwa navyo. # namna ya kula wakati wa shibe na jinsi ya kula wakati wa njaa, yaani vingi na kuwa mhitaji Ki-msingi sentensi hizi mbili zinamaanisha kitu kile kile. Paulo huzitumia kusisitiza kuwa amejifunza kurithika katika mazingira ya namna yeyote ile. # Ninaweza kufanya haya kwa kuwezeshwa na yeye anitiaye nguvu. "Naweza kufanya mambo yote kwa sababu Kristo hunipa nguvu"