# kambini Hii ni sehemu wanaokaa maaskari. # kikosi "Idadi kubwa" au "wengi" # Wakamvika Yesu vazi la zambarau Hii ilikuwa tendo la kejeli. Zambarau ilikuwa rangi inayoonesha mamlaka na kumvalisha ni namna ya kudhihaki cheo chake, "Mfalme wa Wayahudi." # Wakaanza kumpigia kumdhihaki na kusema, "salaam, Mfalme wa Wayahudi!" Maaskari walimdhihaki Yesu kwa sababu hawakuamini kwamba alikuwa Mfalme wa Wayahudi.