# Kama uko tayari? Yesu anakemea wasiwasi wa mtu. Hii swali linaweza kuandikwa tofauti au kama sentensi. "Yesy akamwambia, "Kwanini unasema, "kama uko tayari"? au " Yesu alimwambia, 'Usingelikuwa umesema. # unaweza Inaweza kuwa msaada kuongeza maelezo yaliyokosekana. "unaweza kufanya lolote" # Kila kitu kinawezekana kwa yeyote aaminiye. Hii inaweza kuandikwa kama dhahania dogo na katika kauli tendaji. "Mungu anaweza kufanya chochote kwa ajili ya watu wanaomwamini yeye" # kwa yeyote "kwa yeyote mtu" # amini Hii inarejea kwa kumwamini Mungu. # Nisaidie kutokuamini kwangu Mwanaume anamuuliza Yesu kumsaidia kushinda kutoamini na kuongezea imani yake. "Nisaidie wakati ninashindwa kuamini" au "Nisaidie kuwa imani zaidi" # kundi linakimbilia kwao Hii inamaanisha kuwa watu zaidi walikuwa wanakimbilia kule aliko Yesu na kundi lilikuwa linakuwa kubwa. # wewe roho bubu na kiziwi Maneno "bubu" na "kiziwi" yanaweza kufafanuliwa. "Wewe roho chafu, wewe unaye sababisha kijana kutokuwa na uwezo wa kusikia na kuongea."