# Sentensi unganishi Wakati Petro, Yakobo, Yohana na Yesu walipokuja chini kutoka mlimani, waliwakuta waandishi wakibishana na wale wanafunzi wengine. # walirudi kwa wanafunzi Yesu, Petro, Yakobo na Yohana walirudi kwa wanafunzi wengine ambao hawakuenda nao mlimani. # waandishi walikuwa wakibishana Waandishi walikuwa wakibishana na wanafunzi ambao hawakuenda pamoja na Yesu. # linashangaa Inaweza kuwa msaada kusema kwanini walishangaa. "walishangaa kwa kuwa Yesu alikuwa amekuja"