# Sentensi unganishi Yesu anaelezea mfano wa udongo kwa wafuasi wake na kisha anawambia kuhusiana na taa kuonyesha vitu vilivyo jificha vitajulikana. # Na akasema kwao "Na Yesu akasema na wanafunzi wake" # Je hamuelewi mfano huu? Mtawezaje kuelewa mifano mingine ? Yesu alitumia maswali haya kuonyesha jinsi alivyokuwa na huzuni kwamba wanafunzi wake hawakuweza kuelewa mfano wake. "kama hautaweza kuelewa mfano huu, fikiri jinsi ilivyo ngumu kwa wewe kuelewa mifano mingine" # Mkulima anayepanda mbegu zake "Mkulima anayepanda mbegu zake huwakilisha" # kwa yule anayepanda neno "Neno" huwakilisha ujumbe wa Mungu. Kupanda ujumbe huwakilisha kufundisha. "yule anayefundisha watu ujumbe wa Mungu" # Baadhi huanguka kandokando mwa njia "Baadhi ya watu ni kama mbegu huanguka kandokando mwa njia" au "Baadhi ya watu ni kama njia ya miguu ambapo mbegu huangukia" # njia "njia ya miguu" # wanapoisikia Hapa wanapo-"i" sikia urejea "neno" au "ujumbe wa Mungu"