# Tuna nini cha kufanya na wewe, Yesu wa Nazareti? Mapepo wanauliza swali wakimaanisha kuwa hakuna sababu ya Yesu kuwaingilia na wanatamani yeye aondoke. " Yesu wa Nazareti, tuache sisi peke yetu! Hakuna sababu ya wewe kutuingilia sisi." # Je! Umekuja kutuangamiza sisi? Mapepo wanauliza swali kumsihi Yesu asiwadhuru. "Usi tuharibu sisi!" # alimtupa yeye chini Hapa neno "yeye" lina rejea kwa mtu aliye pagawa na mapepo. # wakati analia kwa sauti kubwa Pepo ndiye anayelia, wala siyo mtu.