# hawa wanakushuhudia nini dhidi yako? "unajibu nini juu ya ushuhuda huu dhidi yako?" # Mwana wa Mungu. Hili ni jina mashuhuri ambalo hueleza uhusiano kati ya Kristo na Mungu. # Mungu aishivyo Tazama 16:13 # Umesema jambo hilo wewe mwenyewe. Yesu anathibitisha kwamba yeye "ndiye Kristo, Mwana wa Mungu. "Kama ulivyosema, Mimi ndiye" au "Umekubaliana na ukweli huo" # Lakini nakuambia, tangu sasa na kuendelea Neno "wewe" ni la wingi. Yesu anamwambia kuhani mkuu na kwa wengine waliokuwapo hapo. # Tangu sasa na kuendelea mtamwona Mwana wa Adamu. Maana zinaweza kuwa: 1) Watamuona Mwana wa Adamu baadaye kwa wakati ujao au 2) kwa "sasa" Yesu anamaanisha wakati wa kifo chake, kule kurudi kwake kutoka kwa wafu, na kupaa kwake kwenda mbinguni. # Mwana wa Adamu Yesu anatumia nafsi ya tatu kuongea juu yake # Upande wa mkono wa kulia wenye nguvu. "Upande wa mkono wa kulia wa Mungu mwenyezi" # Akija katika mawingu ya mbinguni. "Akisafiri kuja duniani katika mawingu ya mbinguni."