# Sentensi unganishi Yesu anaendelea kueleza mfano wa watumishi na talanta # na baada ya muda Kirai hiki kimetumika kuonesha mwanzo wa habari mpya. Yesu anaanza kueleza sehemu mpya ya simulizi. # Nimepata talanta tano zaidi "Nimepata faida ya talanta tano zaidi." # Talanta Mali yenye thamani kubwa. talanta moja ilikuwa sawa na mishahara ya miaka ishirini.Tazama tafsiri katika. 25:14--15. # Hongera. "Umefanya kazi vizuri." au "Umefanya vema." Katika utamaduni wako pengine mnao usemi ambao mkuu (mtu mwenye mamlaka) angetumia kuthibitisha kile ambacho mtumishi wake (au yeyote chini yake) amekitekeleza. # Ingia katika furaha ya Bwana wako "Njoo ufurahie na mimi"