# uovu utaongezeka "watu watafanya dhambi zaidi na zaidi" # Upendo wa wengi utapoa. Maana ya karibu: 1."watu wengi hawatawapenda wenzao." au 2."watu wengi hawatampenda Mungu." # atakayevumilia "yeyote atayebaki na uvumilivu" # mpaka mwisho haieleweki kama "mwisho" inamaanisha mtu anapokufa, au wakati dhiki itakapokoma, au mwisho wa nyakati wakati Mungu atakapojionesha kuwa mfalme. jambo l a kuzingatia hapa ni uvumilivu usiokoma # ataokolewa "Mungu atamwokoa mtu huyo" # Hii injili ya ufalme itahubiriwa "Watu watahubiri ujumbe juu ya utawala wa Mungu" # Mataifa yote. "Watu wote katika sehemu zote." # na ndipo ule mwisho "mwisho wa ulimwengu" aua "mwisho wa nyakati"