# Hosana Neno la Kiebrania linalomaanisha "Tuokoe" lakini pia linaweza kumaanisha "Kumsifu Mungu!" # Mwana wa Daudi Yesu hakuwa mwana halisi wa Daudi, kwa hiyo hii inaweza kutafsiriwa kama "kizazi cha mfalme Daudi. Lakini pia, "Mwana wa Daudi" ni cheo cha Masihi, Huenda makutano walikuwa wakimwita Yesu kwa cheo hiki. # kwa jina la Bwana Hapa "kwa jina la Bwana" inamaanisha "kwa nguvu ya Bwana" au "kama mwakilish wa Bwana" # Hosana juu zaidi Neno "juu zaidi" linamaanisha Mungu atawalaye kutoka juu mbinguni. "Mungu asifiwe, ambaye yuko juu mbinguni" au "Sifa kwake Mungu" # Mji mzima ulitaharuki Neno "mji" linamaanisha wakazi wa mji huo. "Watu wengi mjini kote walitaharuki"