# Tazama Neno hili linatutayarisha kuwa tayari kwa taarifa za kushangaza zinazofuata. # kwao kwa wanafunzi waliokuwa na Yesu amabao ni Petro, Yakobo na Yohana # akajibu na kusema "sema." Petro hajibu swali. # pamoja naye "pamoja na Yesu" # ni vizuri kwetu kuwa hapa Maana zinazowezekana: 1)"ni vizuri kwamba sisi wanafunzi tuko hapa pamoja nawe, Musa, na Eliya au 2)"ni vizuri kuwa wewe, Musa, Eliya, na sisi wanafunzi wote tuko hapa pamoja" # mahala pa kujihifadhi Maana zinazowezekana: 1)mahali pa watu kuja kuabudia au 2)mahali pa muda pa watu kulala.