# Sentensi unganishi Yesu anaendelea kujibu hoja za mafarisayo za kwamba alimponya mtu kwa nguvu za shetani # ikiwa shetani atamwondoa shetani mwenzake Matumizi ya pili ya shetani yanamaanisha pepo wanaomtumikia shetani. "Kama shetani atafanya kazi kinyume na pepo zake" # Shetani ... Beelzabul Majina yote yanamaanisha nafsi moja # ufalme wake utasimama? Yesu anatumia swali kwapa changamoto Mafarisayo. "Ufalme wa shetani hauwezi kusimama" au "ufalme wa shatani hautadumu" # wafuasi wenu huwatoa kwa njia ya nani Yesu anatumia swali lingine kuwapa changamoto Mfarisayo. "kisha lazima useme wafuasi wenu pia huwatoa pepo kwa nguvu za beelzabul. Lakini mnajua kuwa hii siyo kweli" # kwa ajili hii watakuwa mahakimu wenu "Kwa sababu wafuasi wenu huwatoa pepo kwa nguvu za Mungu, wanahakikisha kuwa mmekosea."