# Sentensi unganishi Yesu anajibu ukosoaji wa mafarisayo # akawaambia Mafarisayo # Hamjasoma ... nao Yesu anatumia swali kujibu ukosoaji wa mafarisayo. Yesu anawapa changamoto ili kufikiri juu ya maana ya andiko ambalo walisoma. "Najua mmesoma juu yaa...nao" # nyumba ya Mungu Wakati wa Daudi bado hapakuwa na hekalu. "hema" au " mahali pa kumwabudia Mungu" # mkate wa wonyesho Huu ni mkate uliotakaswa ambao makuhani walipeleka mbele za Mungu hemani. "Mikate ambayo makuhani walipeleka mbele za Mungu # wale aliokuwa pamoja nao "watu waliokuwa pamoja na Daudi" # ila halali kwa makuhani "ni makuhani tu walioruhusiwa kuula."