# Sentensi unganishi. Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake kuhusu kutohofia dhiki itakayowakabili. # Yeye atakaye Neno "yeye" linamaanisha mtu yeyote. "yeyote" au "yeyote ambaye" au " ambaye" # atakayewakaribisha Inamaanisha kumkaribisha mtu kama mgeni # Wa Kiwakilishi "wa" kinamaanisha mitume kumi na wawili ambao Yesu anawaaambia. # ananikaribisha mimi Yesu anamaanisha ni sawa na kumkaribisha yeye. "ni kama ananikaribisha mimi" au "ni kama vile alikuwa ananikaribisha mimi" # kumkaribisha yeye aliyenituma Hii inamaanisha wakati mtu anamkaribisha Yesu ni sawa na kumkaribisha Mungu. "ni kama vile kumkaribisha Mungu aliyenituma" # Kwa sababu ni nabii Hapa kiwakilishi cha "ni" kinamaanisha mtu anayekaribishwa. # thawabu ya nabii Hii inamaanisha zawadi ambayo Mungu anampa nabii. wala siyo zawadi ambayo nabii anampatia mtu mwingine. # mtu wa haki Hapa "wa" haimaanishi mtu anayekaribisha. Inamaaanisha mtu anayekaribishwa. # thawabu ya mtu wa haki Hii inamaanisha zawadi ambayo Mungu humpa mtu wa haki, siyo zawadi ambayo mtu wa haki humpatia mtu mwingine.