# Sentensi unganishi Hii inaanzisha habari ya Yesu akiwaponya wanaume wawili waliokuwa vipofu # Alipokuwa akipita Yesu njiani Yesu alikuwa akiondoka kwenye mji # akipita "Alikuwa akiondoka" au "alikuwa akienda" # wakamfuata Hii inamaainisha kuwa walikuwa wakitembea nyuma ya Yesu, siyo lazima kuwa walikuwa wameshakuwa wanafunzi wake. # uturehemu Inamaanisha kuwa walitaka Yesu awaponye # Mwana wa Daudi Yesu hakuwa mwana halisi wa Daudi, hivyo inaweza kutafsiriwa kama "Ukoo wa Daudi". Ingawa, "Mwana wa Daudi" pia ni cheo alichopewa Masihi, na wale wanaume yawezekana walikuwa wakimwita Yesu kwa Sifa hii. # Pindi Yesu alipokuwa amefika kwenye nyumba Hii inaweza kuwa nyumba ya Yesu au nyumba iliyosemwa kwenye 9:10 # Ndiyo,Bwana Jibulote halijatolewa lakini linaeleweka "Ndiyo, Bwana, tunaamini kuwa unaweza kutuponya."