# Sentensi unganishi Hii inahitimisha simulizi la Yesu la kumfufua binti wa afisa wa Kiyahudi # Maelezo kwa ujumla Mstari wa 26 unatoa muhtasari unaofafanua matokeo ya Yesu kumfufua huyu msichana. # Na wale watu walipotolewa nje "Baada ya yesu kuwatoa watu nje" au "Baada ya familia kuwatoa watu nje" # akaamka "akaamka kutoka kitandani" Hii ni maana ile ile kama iliyo kwenye 8:14 # Habari hii ikaenea mji mzima Watu wote wa mji ule walisikia kuhusu hilo" au "Watu walioona binti akiwa hai walianza kuwaambia watu wa eneo hilo habari hizi."