# Sentensi unganishi Hii inarudisha habari ya Yesu kumfufua binti wa afisa wa Kiyahudi # nyumba ya ofisa Hii ilikuwa nyumba ya kiongozi wa kiyahudi # wapiga tarumbeta na umati wa watu walikuwa wakipiga kelele Huu ni utamaduni wa kawaida wa kumboleza pale mtu anapokuwa amekufa. # wapiga zumari "watu ambao wanapiga zumari/filimbi" # Ondoka hapa Yesu alikuwa akiongea kwa watu wengi, hivyo tumia mfumo wa wingi wa kutoa amri kama lugha yenu inao huo. # binti hajafa, lakini amelala Yesu anatumia igizo la maneno. Ilikuwa ni kawaida kipindi cha Yesu kusema mtu aliyekufa kuwa "amelala" Lakini hapa binti aliyekufa ataamka, ingawa yeye alikuwa amelala.