# Sentensi unganishi Hii inaanzisha simulizi ya Yesu kumfufua binti wa afisa wa Kiyahudi baada ya kufa. # mambo hayo Hii inarejea jibu la Yesu alilowapa wanafunzi wa yohana kuhusu kufunga. # Tazama Neno "tazama" linatupa dokezo la mtu mwingine mpya katika hadithi. Lugha yako inawezekana ikawa na njia nyingine ya kufanya hivi. # akasujudu kwake Hii ni njia mtu yeyote kuonyesha heshima katika utamaduni wa kiyahudi. # njoo na uweke mkono wako juu yake, na yeye ataishi tena Hii inaonyesha kwamba ofisa wa kiyahudi aliamini Yesu ana nguvu ya kurudisha uhai wa binti yake. # wanafunzi wake wanafunzi wa Yesu