# Sentensi unganishi Hii inahitimisha habari ya Yesu ya kumponya mtu aliyepooza. Kisha Yesu akamwita mtoza ushuru kuawa mmoja wa wanafunzi wake. # ambaye amewapa "kwa sababu amewapa" # mamlaka hayo mamlaka ya kuthibitisha kusamehe dhambi # Na Yesu alipokuwa akipita kutoka hapo Kirai hiki kinaonyesha mwanzo wa simulizi mpya. Kamalugha yako ina namna ya kufanya hili, unaweza kulitumia mahali hapa. # akaipita kutoka hapo "alikuwa akiondoka" au "alikuwa akienda" # Mathayo...naye...Yeye Utamaduni wa kanisa unasema Mathayo ni mwandishi wa hii Injili, lakini andiko halitoi sababu ya kubadilisha kiwakilishi kutoka "naye" na "yeye" kwa "kwangu" na "mimi" # Yeye alisema naye "Yesu alisema na Mathayo" # naye akamwambia "Yesu alimwambia Mathayo" # Naye akasimama na kumfuata yeye "Mathayo alisimama na kumfuata yeye" kama mwanafunzi, siyo tu kujumuika na Yesu kwa kinachofuata kukamilisha.