# Sentensi unganishi Mwandishi anarejea kwenye wazo kuu, ambalo linaanzia 8:1, la Yesu akiwaponya watu. Hii inaanzisha habari ya Yesu akimponya mwanamume aliyekuwa amepooza # Yesu akaingia kwenye boti Wanafunzi yamkini walienda na Yesu' # boti Yamkini ni boti ile ile # akafika kwenye mji wake "mji ambao yeye aliishi" # Ndipo Hii inaonyesha mwanzo wa tukio jingine kubwa la hadithi. Linaweza kuhusisha watu wengine tofauti na tukio lililopita. Lugha yako inaweza kuwa na njia nyingine ya kuonyesha hili. # yao....zao Hii inaonyesha wale ambao walimleta mgonjwa wa kupooza kwa Yesu. Hii inahusisha mgonjwa aliyepooza mwenyewe. # Mtoto Huyu mtu hakuwa mtoto halisi wa Yesu. Yesu alikuwa akiongea naye kwa upole. Ikiwa hii inachanganya, inaweza pia kutafsiriwa"Rafiki yangu" au "Kijana" au hata kuondolewa. # Dhambi zako zimesamehewa "Mungu amesamehe dhambi zako" au "Nimekusamehe dhambi zako"