# Sentensi unganisha Hapa simulizi linabadilika na kusimulia jinsi Yesu alivyosema juu ya watu waliotaka kumfuata # Kisha Hili neno limetumika hapa kuonyesha alama ya kikomo cha hadithi. Hapa Mathayo anaanza kueleza sehemu mpya ya hadithi. # yeye alitoa maelekezo "aliwaambia wanafunzi wake" # Ndipo Hapa inamaanisha baada ya Yesu "kutoa maelekezo" lakini kabla yake kuingia ndani ya boti. # popote "sehemu yeyote" # Mbwea wana mashimo, na ndege wa angani wana vichari Hii ina maana hata wanyama wakali wana sehemu ya kupumzika. # mbwea Mbwea ni wanyama kama mbwa. Wanakula ndege wadogo na wanyama wengine wadogo. Ikiwa mbwea hawajulikani kwenye eneo lako, tumia kwa ujumla mbwa - kama viumbe au mnyama mwingine mkali. # shimo Mbwea wanatengeneza mashimo ardhini kwa kuishi humo. Tumia neno sahihi kwa eneo ambalo mnyama "mbwea" anaishi. # mwanadamu Yesu anaongelea kuhusu yeye mwenyewe # hana sehemu ya kulaza kichwa chake Hii ina maanisha sehemu ya kulala. "hana sehemu yake ya kulala."