# Sentensi unganishi Huu ndio mwisho wa mahubiri ya Yesu ya mlimani yanayoanzaia 5:1 # atafananishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga Yesu aliendelea kutumia mlinganyo kutoka mstari uliopita. Yeye analinganisha wale ambao hawatii neno lake na mpumbavu aliyejenga nyumba. Mpumbavu pekee aweza kujenga nyumba juu ya mchanga ambapo mvua,mafuriko na upepo vinaweza kuhamisha mchanga. # kuanguka Tumia neno la ujumla kwa lugha yako ambalo linaelezea kilichotokea wakati nyumba inaanguka chini. # na anguko lake likakamilika Mvua,mafuriko na upepo hakika yaliangamiza nyumba.