# Sentensi unganishi Yesu anaanza kufundisha juu ya fedha na mali # Maelezo kwa ujumla Yesu anawaambia makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye katika maisha yao binafsi. viwakilishi vya "usi" na "yako" viko katika wingi isipokuwa vile vya mstari wa 21, amabvyo viko katika umoja. # akiba "utajiri" # ambapo nondo na kutu wanakula "ambapo nondo na kutu wanashambulia akiba" # nondo mdudu mdogo, anayeruka na kuharibu nguo # kutu ni vitu vya rangi ya kahawia vinavyopatikana kwenye chuma # weka akiba yako mbinguni Huu ni msemo ambao unamaanisha kwamba fanya mambo mazuri hapa duniani ili Mungu akubariki mbinguni. # na moyo wako utakapokuwepo pia. Hapa "moyo" maana yake ni mawazo ya mtu na mapenzi yake.